Hatimaye Kocha Roberto Mancini amesema sababu iliyochangia kumkwida Mario Balotelli wakati wote wakiwa wafanyakazi wa Manchester City ya England mwaka 2013.
Picha zilizagaa mitandaoni wakiwa wanavutana huku Mancini raia wa Italia akionekana kuwa na jazba.
Lakini katika mahojiano na gazeti moja la Ufaransa, Mancini amesema alikasirishwa na tabia ya Balotelli ya kutosikiliza.
“Niliwaambia wachezaji wote, wawe makini na wenzao ambao walikuwa ni wagonjwa, wacheze kwa uangalifu.
“Mfano Gael Clichy alikuwa ndiyo ametoka kwenye majeruhi. Nilisisitiza, lakini ajabu Balotelli hakusikia, akamrukia. Nilikasirishwa sana kwa kweli,” alisema.
“Lakini kuhusiana na picha zile, hakukuwa na mvutano mkubwa sana kama ilivyozagaa. Nilimvuta, nikataka kumuangusha lakini alikuwa imara sana kuliko mimi, sikuweza. Lakini kweli nilikasirika sana.”
0 COMMENTS:
Post a Comment