October 10, 2016

MWALUSAKO
Beki wa zamani wa Yanga, Lawrance Mwalusako amewashukia Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na kuwataka wawe makini katika suala la mabadiliko wanayotaka kufanya Yanga.

Mwalusako ambaye pia aliwahi kuwa katibu mkuu wa Yanga, amewaambia BMT kuwa, kuendesha timu gharama na wajue Yanga wameridhia wenyewe.

Hivi karibuni, BMT kupitia Katibu wake, Mohamed Kiganja imeibuka na kuyazugumzia mabadiliko ya Yanga kutaka kukodisha inagwa imeonekana kujichanganya sana katika hilo kwa kuwa mengi inayotaka yafanyiwe kazi, yaliishafanyiwa kazi.

“Katika hili BMT naona hawapo sawa kwa sababu Yanga ina haki yake ya kujiamulia mambo yake kwa ajili ya manufaa yake.

“Inashangaza sana kila linapokuja jambo fulani BMT wanaingilia lakini katika michezo mingine hawafanyi hivyo wakati huko ndiko kuna madudu mengi.

“Hakika hii siyo sawa kwani kuendesha timu siyo jambo rahisi hata kidogo, mimi nimekuwa kiongozi pale Yanga, najua matatizo yaliyomo ndani ya klabu hiyo yanayohusu uchumi, sasa kapatikana mtu ambaye atasaidia mambo kuwa sawa tunampinga! Katika hili siwaungi mkono BMT.


“Waliokuwa wanatakiwa kupiga kelele ni TFF, Caf na Fifa ambao ndiyo wenye jukumu la kusimamia soka kama mfumo huu wa kukodishwa timu haufai na siyo BMT.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic