October 24, 2016Kocha Hans van der Pluijm ameachia ngazi rasmi kuinoa Yanga.

Pluijm ameamua kuachana na Yanga na barua yake ameikabidhi na uongozi wa Yanga tayari umemjibu.


Hii ni baada ya kamati ya Mashindano ya Yanga kuamua kumleta Kocha George Lwandamina raia Zambia.

Tayari Mzambia huyo yupo jijini Dar es Salaam akiendelea na mazungumzo na uongozi wa Yanga.

Kumekuwa na taarifa wameishamalizana lakini uongozi wa Yanga umeendelea kusema ni mazungumzo tu.

1 COMMENTS:

  1. Sare ya WEKUNDU imemletea taabu mzee wa watu...tuna safari ndefu sana Wabongo..katikati ya ligi kocha anajiuzulu????naamini haya ni maamuzi ya mtu mmoja tu maana haiwezekani ghafla hivi.....kweli zidumu fikra za MWENYECHAIR...

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV