October 9, 2016Mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Jerry Tegete ameipiga kumbo klabu yake hiyo ya zamani na kutakiwa imlipe kitita chake cha Sh milioni 10.

Taarifa kutoka ndani ya TFF, zimesema Tegete ambaye sasa anakipiga Mwadui inatakiwa alipwe fedha hizo ambazo zinatokana na Yanga kuvunja mkataba wake pamoja na fedha nyingi ambazo ni zake.

SALEHJEMBE, ilimtafuta Tegete ambaye alisema kweli katika moja ya kamati iliyokaa kusikiliza suala hilo, imeamua hivyo.

“Wameamua nilipwe kwa kuwa ni haki yangu,” alisema.

Pamoja na Tegete wengine waliotakiwa kulipwa ni Omega Seme ambaye pia alikuwa akidai.


Kawaida, klabu nyingi zimekuwa zikiingia kwenye mgogoro na wachezaji kutokana na suala la mikataba na hasa wakati wa kuvunja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV