October 10, 2016Friends Rangers jana imeonyesha hasira zake baada ya kuichapa Ashanti bao 1-0 katika mchezo mkali wa Ligi Daraja la Kwanza uliochezwa kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.

Shujaa wa vijana hao wa Magomeni, alikuwa ni Fabo Yusuph Mkinda aliyefunga bao hilo pekee na kuwafanya mashabiki wa Friends waibue shangwe kubwa.

Ushindi huo unawafanya washkaji hao kufikisha pointi nne huku wakiendelea kuchuana vikali kuhakikisha wanapanda hadi Ligi Kuu Bara msimu ujao.

Hii ni mechi ya tatu kwa Friends, mchezo wa kwanza walifungwa mabao 5-0 na Mshikamano ambayo pia ni ya Dar, kisha mechi ya pili wakasuluhu na Pamba ya Mwanza. Mechi zote imecheza jijini Dar es Salaam.

Ligi Daraja la Kwanza imeshika kasi kwenye viwanja mbalimbali Tanzania Bara huku ushindani ukionekana kuwa mkubwa kwelikweli.  

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV