October 24, 2016Mshambuliaji Thomas Ulimwengu amesema anataka kucheza Ulaya na si TP Mazembe tena.

Ulimwengu amemaliza mkataba wake na TP Mazembe na tayari amerejea nchini akisubiri mipando ya kwenda kucheza barani Ulaya.

Meneja wa Ulimwengu, Jamal Kisongo amesema kuna timu zinamtaka Ulaya lakini hawawezi kubainisha sasa.

“Mpango wa kwenda Ulaya ulikuwa ni wa muda mrefu sana, lakini sasa ndiyo wakati mwafaka.

“Siwezi kukuambia nchi kwa sasa, lakini tunachoangalia hapa ni Ulimwengu kwenda kucheza huko, ndiyo wakati wenyewe,” alisema Kisongo.


Kisongo ambaye pia ni Meneja wa Mbwana Samatta, amekiri kuwa kweli mkataba wa Ulimwengu na Mazembe umefikia tamati.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV