November 18, 2016Pamoja na uongozi wa Simba kuwawekea ngumu wachezaji wake kucheza mechi za mchangani, mastaa wa timu hiyo mshambuliaji, Ibrahim Ajibu na kiungo Said Ndemla katikati ya wiki hii waliichezea timu ya Kunduchi Sport katika michuano ya Kombe la Tegeta Cup dhidi ya Napoli FC.

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari Tegeta, Dar, Kunduchi Sport ilijikuta ikiambulia kichapo cha mabao 2-0 licha ya uwepo wa wachezaji hao pamoja na kiungo wa Mwadui FC, Abdallah Seseme na mshambuliaji wa Stand United, Kelvin Sabato.

Ikumbukwe kuwa uongozi wa Simba ulishapiga marufuku wachezaji wake kujihusisha na mashindano ya mchangani kwa kuhofia kupata majeraha yasiyokuwa ya lazima, lakini wachezaji hao wamekaidi agizo hilo.

Mratibu wa michuano hiyo, Justin Ilanfya amesema: “Licha ya Kunduchi Sport kuamua kuwaleta mastaa kibao wa ligi kuu lakini hawakuweza kusaidia chochote kufuatia kupokea kipigo cha aibu kutoka kwa Napoli.


 “Walikuwa na wachezaji wa Simba ambao ni Ajibu na Ndemla, Seseme wa Mwadui na yule Sabato kutoka Stand wote hawakuweza kuwasaidia kitendo kilichowashangaza mashabiki wengi kutokana na uwezo wa wachezaji hao.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV