November 18, 2016


Pamoja na yeye kuahidi kurejea Yanga kwa kasi, klabu nne za Ligi Kuu Bara zikiwemo Stand United, Tanzania Prisons, JKT Ruvu na Mtibwa Sugar zimejikuta zikigongana katika Klabu ya Yanga kumuwania mshambuliaji Malimi Busungu kwa ajili ya kumsajili kwenye dirisha dogo la usajili linaloendelea hivi sasa.

Busugu aliingia mgogoro na benchi la ufundi la timu hiyo na kuamua kutimka kikosini hapo kutokana na kutopata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza.

Meneja wa Busungu, Yahya Tostao, amesema hadi sasa Yanga haijawapa taarifa yoyote juu ya kuendelea ama kuachana na mchezaji huyo huku wakiwa wamepokea barua kutoka katika timu nne za ligi kuu.

“Bado Yanga haijatupa taarifa yoyote juu ya kuendelea ama kutoendelea na Busungu, hivyo tunawasubiri wao iwapo watahitaji kumtoa kwa mkopo basi tutazungumza nao kuweza kujua maslahi ya mchezaji,” alisema Tostao.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV