November 17, 2016


Pamoja na kwamba kumekuwa na taarifa kuwa Yanga haitaacha hata mchezaji mmoja, taarifa zinasema wachezaji walioonekana hawana faida, watakutana na panga.

Wachezaji ambao hawakucheza mechi nyingi na walionekana mchango wao haukuwa mkubwa, wataachwa ili kupisha nafasi wakati Yanga inaongeza wachezaji.

“Mchakato unaendelea, Yanga imekuwa ikifanya mambo yake kitaalamu sana. Kuna wachezaji wataachwa, hii ni lazima,” kilieleza chanzo.

“Hata katika hali ya kawaida kabisa, unawaona wako ambao hawakuwa na mchango kabisa. Hata wao wanaliona hilo na hawatalaumu.”


Yanga sasa iko katika nafasi ya pili baada ya kumaliza vizuri mzunguko wa kwanza na kuipa Simba presha kubwa. Kwani awali Msimbazi walikuwa wanaongoza kwa toafauti ya pointi na sasa ni hizo mbili tu baada ya Simba kupoteza mechi mbili za mwisho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV