November 16, 2016
Kampuni ya StarTimes imezidi kupaa kiteknolojia baada ya kuzindua runinga mpya ambazo king'amuzi kipo ndani ya runinga.

Runinga hizo zenye ukubwa wa Inchi 40, 32 na 24 zina king'amuzi ambacho kinakuwa ndani yake na bado unaweza kuunganisha kingine ukitaka.

Runinga ya Inchi 40 ni Sh 750,000, ya Inchi 32 ni Sh 500,00 na ndogo ni Inchi 24 ni Sh 320,000, bei ambazo zimeonekana ni nafuu na Watanzania wengi wenye kipato cha kati hata cha chini wanaweza kuzinunua.

Kinachovutia zaidi ni kwamba runinga hizo, ndani yake zina king'amuzi hivyo atayenunua hahitaji kununua king'amuzi cha StarTimes.

1 COMMENTS:

  1. Hamna unafuu hapo kwa sabubu inch 40 kariakoo ni 600,000 mpaka 620,000 na inch 32 400,000 mpaka 420,000. Sasa kwa inch 40 kunatofauti ya 150,000. Swali je king'amuzi cha startimes ndio kinauzwa 150,000 jibu ni hapana.

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV