November 17, 2016


Kocha George Lwandamina, anaamini kuangalia mikanda kadhaa ya DVD kutamsaidia kukisoma kikosi chake kipya.

Awali, Lwandamina alisema hawezi kuwaacha wachezaji katika kikosi chake wakati hajawahi kuwaona wakicheza.

“Naendelea kusubiri DVD, nikizipata nitaangalia na kujua nini cha kufanya. Siwezi kusema ninaleta mchezaji mpya au ninamuacha bila ya kuona,” alisema.

Kocha huyo mtaratibu, aliishuhudia mechi ya mwisho ya Ligi Kuu Bara, wakati Yanga ilipocheza na Ruvu Shooting ambayo Yanga ilishinda kwa mabao 2-1.


Lwandamina ndiye kocha mpya wa Yanga ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili kuinoa akitokea katika klabu ya Zesco ya Zambia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV