November 17, 2016


Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema tayari walishamalizana na wachezaji ambao wamekuwa wakizungumzwa kuhamia Yanga.

Kiungo Jonas Mkude na beki Hussein Zimbwe Jr, ni kati ya wachezaji wamekuwa wakihusishwa na kujiunga na Yanga.

Hans Hoppe amesema Simba inajua inachokifanya ni kumalizia vitu vichache tu na wachezaji hao.

“Kila kitu tulishazungumza na kumalizana, kuna mambo madogomadogo sana yanatakiwa kumaliziwa,” alisema Hans Poppe.

“Sasa hao wanaosema maneno mengi, sisi tunaendelea na mambo yetu na si kusikiliza wanasema nini."

Taarifa nyingine zinaeleza, uongozi wa Simba kupitia Hans Poppe umeanza kukutana na wachezaji hao.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV