November 12, 2016



Baada ya Yanga kumalizana na Kocha Mzambia George Lwandamina, imeelezwa anatarajia kuanza kazi mara tu mapumziko waliyopewa wachezaji kwisha.

Kila kitu kati ya kocha huyo kimemalizika jana jioni na sasa ni yeye tu kuanza kazi.

Jana jioni kikosi kizima cha Yanga kiliitwa ofisini kwa mwenyekiti wa timu hiyo, Yusuf Manji na kulipwa fedha za malimbikizo ya usajili na mshahara wa Oktoba ambao walikuwa hawajalipwa.

Uongozi wa Yanga umepanga kumalizana na kila mchezaji ili kuweka sawa kikosi chao ambacho kinatetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa mara ya tatu mfululizo.

“Tumeitwa ofisini kwa mwenyekiti ili tukalipwe madai yetu ikiwemo fedha za usajili na mshahara wa mwezi wa kumi ambazo tulikuwa bado hatujalipwa.

“Tunaona mambo yanakuwa mazuri na tutaenda likizo tukiwa na furaha hivyo tukirejea tutaendelea na ligi tukiwa na amani kubwa moyoni,” alisema mmoja wa wachezaji wa Yanga ambaye aliomba hifadhi ya jina lake kutokana na usiri wa jambo hilo.

Wakati hayo yakitokea, Yanga juzi iliingia mkataba wa miaka miwili na Lwandamina ambaye ni kocha wa zamani wa Zesco ya Zambia ambaye aliipa ubingwa mara mbili mfululizo timu hiyo ya Zambia.

“Kocha ameshasaini mkataba wa miaka miwili na tutakuwa naye kuanzia mzunguko wa pili wa ligi,” alisema bosi huyo mwenye nguvu kubwa ya ushawishi ndani ya Yanga.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic