November 12, 2016



Mwili wa Spika wa zamani wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania, Samuel Sitta uliagwa jana jijini Dar es Salaam na Dodoma ambapo leo utazikwa kwao wilayani Urambo mkoani Tabora.

Sitta, 74, alifariki dunia Jumatatu wiki hii nchini Ujerumani alikokuwa akitibiwa ugonjwa wa saratani ya tezi dume na mwili wake uliwasili nchini juzi na jana uliagwa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli aliwaongoza mamia ya waombolezaji wakiwemo wanasiasa, viongozi wa serikali na wananchi kuuaga mwili wa Sitta kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

Baadaye mchana mwili wa Sitta ulisafirishwa hadi mjini Dodoma ambapo jioni uliagwa Bungeni.

 Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Hassan Dalali amesema kifo cha Sitta ni pigo kubwa kwa Simba kutokana na mchango wake katika timu.

Katika hotuba yake fupi wakati wa kuuaga mwili huo Bungeni Dodoma, Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT), Zitto Kabwe alisema: “Mzee Sitta alikuwa mwanamichezo na mwanachama wa Simba, huyu aliipeleka Simba nchini Brazil mwaka 1982 kwa ajili ya kambi.


“Timu iliporudi Brazil ikaifunga Yanga mabao 5-0 na tangu hapo Simba imekuwa ikitoa vipigo vya aina hiyo na hadi leo Yanga haijawahi kuvunja rekodi hiyo hata kwa kuungaunga, hakika hili ni pigo kwa Simba.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic