November 13, 2016

CHIRWA AKIPAMBANA NA AGGREY MORRIS WA AZAM FC


Mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa amesema ataendelea kujifunza na kujiimarisha pia kwa ajili ya Ligi Kuu Bara, mzunguko wa pili.

Lakini amesisitiza kwamba pamoja na ushindani kisoka, bado kuna wachezaji wanapaswa kuelekeza nguvu kwenye ushindani sahihi ili kukuza mpira wa Tanzania.

"Kweli ligi ni ngumu, inahitaji ubunifu na kujituma, wachezaji wengine pia waongeze kiwango chao na kupambana kwa lengo la ushindani halali.

"Kukiwa na ushindani halali, kunasaidia kukuza mchezo kwa ushindani," alisema Chirwa ambaye alianza ligi hiyo vibaya kabla ya kucharuka na kuanza kuonyesha cheche.

Pamoja na kwamba Chirwa hakutaka kufunguka sana kuhusiana na ushindani sahihi, alionyesha wazi anazungumzia mabeki wa timu alizokutana nazo kulenga katika ushindani wa kimchezo na si nje ya hapo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic