Mshambuliaji nyota wa Chelsea, Eden Hazard amesema asingependa kuwa nahodha wa Chelsea kama ilivyo kwa John Terry.
Hazard amesema hatauweza unahodha kwa kuwa yeye si mtu anayezungumza sana kama ilivyo kwa Terry hasa wakati wa kuhamasisha.
“Sidhani kama nitaweza kama ilivyo kwa Terry, yeye ana uwezo wa kuzungumza. Mimi siwezi kabisa.
“Kawaida yang nimekuwa nikizungumza na miguu yangu uwanjani ifanye kipi ambacho ni sahihi,” alisema.
Hazard aria wa Ubelgiji, amerejea katika kiwango kizuri na sasa anaonekana kuwa tegemeo la uzalishaji na ufungaji mabao katika kikosi cha Chelsea.
0 COMMENTS:
Post a Comment