November 14, 2016


CHAILA (KULIA)...

Baada ya kocha George Lwandamina kumalizana na Yanga, mchezaji wa kwanza ambaye ataungana naye anaonekana kuwa ni Meshack Chaila kutoka Zesco ya Zambia.
Taarifa zinaeleza, Yanga tayari wamefanya mazungumzo ya awali na kukubaliana na Chaila raia wa Zambia ambaye hiyo karibuni ametoka kwenye fungate baada ya kufunga ndoa.
Imeelezwa kiungo huyo, kakubali kusaini mkataba wa miaka miwili ili aungane na Lwandamina.
Chaila ni kiungo mkabaji na mtu wa kazi, sehemu ya kiungo ambayo Yanga wamekuwa na tatizo nayo kwa kipindi sasa.
Lwandamina aliyekuwa kocha mkuu wa Zesco, akiwa bosi wa Chaila, tayari amemalizana na Yanga na hivi karibuni ataanza kazi.
 Chaila amethibitisha kufanya mazungumzo na Yanga: “Wamezungumza na meneja wangu, mambo yako katika hatua nzuri na ikiwezekana Novemba 15 nitajiunga nao. Hapa Zesco hawana shida kumuachia mchezaji.”

Chaila ambaye alizungumza na mtandao wa Soka25 East, ameonyesha yuko tayari kujiunga na Yanga na kufanya kazi na Lwandamina.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV