November 10, 2016



Mshambuliaji nyota wa Simba, Shiza Kichuya amesema wachezaji wa Prisons waliwapania kupita kiasi.

Simba imepoteza mechi yake ya pili ya Ligi Kuu Bara baada ya kuchapwa mabao 2-1 na Prisons ya Mbeya, jana.

Simba imefungwa ikiwa ni mechi ya pili mfululizo inapoteza baada ya kuwa imetoka kupoteza mechi dhidi ya African Lyon.

“Mechi ilikuwa ngumu lakini tulicheza vizuri tu. Tatizo wachezaji Prisons walitupania sana,” alisema Kichuya ambaye ni kati ya viungo bora wa Ligi Kuu Bara kwa msimu wote wa kwana uliopita.


Pamoja na kufungwa, bado Simba ilipoteza nafasi nzuri kadhaa za kufunga ambazo zingeiwezesha kuibuka na ushindi au kupata sare.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic