November 7, 2016

MO IBRAHIM

Bosi wa benchi la ufundi la Simba, Mcameroon, Joseph Omog, ataendelea kumpa nafasi kiungo wake mshambuliaji, Mohammed Ibrahim kwenye kikosi chake huku akimtaka Ibrahim Ajibu kuongeza bidii ili arejee kikosini.
Kauli hiyo, aliitoa hivi karibuni kwenye maandalizi ya mwishoni kuelekea mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya African Lyon iliyochezwa jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Awali, Ajibu alikuwa akianza kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo huku Mohammed akianzia benchi, lakini katika mechi za hivi karibuni mshambuliaji huyo aliyekuwa tegemeo amejikuta akianzia benchi.
OMOG

Omog alisema ni ngumu kumuweka benchi Mohammed na kumuanzisha Ajibu kutokana na kiwango kikubwa kinachoonyeshwa na kiungo huyo aliyetua kuichezea timu hiyo msimu huu akitokea Mtibwa Sugar.
Omog alisema, yeye sera yake kwenye timu huwa anampa mchezaji nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza kutokana na kiwango, kujituma na bidii yake uwanjani, lakini siyo kumfurahisha.
AJIBU

"Kama unavyokiona kikosi changu, kina wigo mpana wa wachezaji wote wenye uwezo mkubwa, kama ikitokea mmoja akaonyesha kiwango kidogo, basi ninamtoa kwenye kikosi cha kwanza na kumuingiza mwingine kama ilivyojitokeza kwa Ajibu.

"Ajibu nilikuwa nikimpa nafasi ya kucheza kutokana na kiwango chake, lakini baada ya hivi karibuni kushindwa kunishawishi kwa kiwango chake kidogo ambacho anakionyesha, nimeona nimtoe na kumuingiza Mohammed ambaye yeye hivi sasa anatoa mchango mkubwa kwenye timu,” alisema Omog.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV