November 25, 2016



Pamoja na kwamba safari ya kiungo wa Azam, Farid Mussa kwenda Hispania katika Klabu ya Tenerife kuonekana kukwama kutokana na kiungo huyo kukosa hati ya kufanya kazi nchini humo, uongozi wa Azam FC umeweka wazi kwamba hauna mpango naye licha ya kwamba hana timu ya kuichezea mpaka sasa.

Farid ambaye aliuzwa na Azam kwenda Tenerife tangu mwanzoni mwa msimu huu wa ligi ulipoanza mpaka sasa ameshindwa kuitumikia timu hiyo inayoshiriki Ligi Daraja la Pili nchini humo kutokana na mabadiliko ambayo yamefanywa ndani ya timu hiyo.

Msemaji wa timu hiyo, Jaffar Idd amesema hawana mpango wa kumsajili Farid kwenye kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo na kumfanya aendelee kubaki hapa nchini kwani wao lengo lao ni kuona winga huyo anacheza soka la kulipwa.

“Ingawa tangu tuachane na Farid katika msimu uliopita na yeye kushindwa kucheza soka kokote pale mpaka sasa lakini katu jambo hilo halitufanyi tumsajili tena mchezaji huyo kwa muda huu kwa sababu tayari kila kitu kimeshakamilika kule kwenye timu yake na kinachosubiriwa ni wao wenyewe tu.

“Lengo letu ni kuona ndoto yake ya kucheza nje ya nchi inatimia na hilo ndilo tunalosimamia sisi na hata kama kwa muda huu ambapo hana timu yoyote ya kuichezea katu sisi hatuwezi kumsajili na kumrudisha kundini.

“Hata Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) sisi tumeshatoa na hapo utaona lengo letu ni kutaka kuona anaondoka na kucheza huko kwa ajili ya kufungua milango kwa wengine kucheza soka la kulipwa,” alisema Jaffar.


SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic