Rais John Pombe Magufuli
ameeleza wazi namna anavyokerwa na tabia za mashabiki kung’oa viti uwanjani
wakati timu zao zinapocheza.
Magufuli amesema amekuwa
akifuatilia michezo, lakini alikerwa kuona mashabiki waking’oa viti.
Mashabiki wa Simba waling’oa
viti wakati timu yao ilipokuwa ikicheza na Yanga.
Magufuli ameyasema hayo wakati
akizungumza na waandishi wa habari Ikulu Dar es Salaam ikiwa ni siku ya
kuadhimisha kutimiza mwaka mmoja tokea aingie madarakani.
“Nafuatilia michezo, napenda. Lakini
nilichukizwa kuona watu wanang’oa viti.
“Waziri alifanya kazi nzuri ya
kuwafungia. Ni vizuri kabisa kwa kuwa hawa watu hawajui uwanja unaotengenezwa
kwa gharama kubwa, wao wanang’oa viti.”
0 COMMENTS:
Post a Comment