Yaya Toure ameamua kuomba radhi kwa klabu yake ya Manchester City kutokana na mgogoro ambao umekuwa ukiendelea kwa muda sasa.
Mgogoro huo umekuwa ukiendelea mara tu baada ya Pep Guardiola kutua Man City akitokea Bayern Munich.
Guardiola ndiye alimuacha Toure akiwa Barcelona, lakini sasa amemkuta akiwa na mafanikio makubwa City, nako ameanza kumuonyesha vituko.
Lakini wakala wa Toure,Dimitri Seluk raia wa Uturuki amekuwa akimshambulia Guardiola mfululizo kuhusiana na suala hilo.
Lakini leo Toure ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook akiomba radhi kwa uongozi wa Man City, mashabiki na wengine. Hata hivyo hakumtaja Guardiola.
“Ninaomba radhi kwa niaba ya wanaoniwakilisha kwa uongozi wa timu na wote wanaofanya kazi kwenye klabu kutokana na hali ya kutokuelewana iliyojitokeza.
“Kauli zilizotolewa haziwakilishi maoni yangu au watu wanaofanya kazi hapa.
“Nina heshima kubwa kwa Manchester City na ninaitakia mema klabu. Nina furaha kuwa sehemu ya historia ya klabu hii. Naishi kwa kucheza soka na kuwaburudisha mashabiki.
“Nawashukuru mashabiki wote kwa ujumbe wao katika kipindi hiki kigumu, hiyo ina maana kubwa kwangu na kwa familia yangu.”
0 COMMENTS:
Post a Comment