November 23, 2016


SUNDAY MANARA

Miaka kadhaa nyuma Baba yangu na shujaa wangu Mohammed Ramadhan Manara(Sunday Manara)Maarufu kama Computer alizaliwa, ninaishuhudia siku hii adhimu kwa my dady na kwangu nikiwa mwenye furaha tele,huku mvua inayonyesha leo ikiongeza furaha hii.


Ndiye Mtanzania pekee uliyecheza na Pele katika kikosi cha New York Cosmo, pia ulicheza na Jomo Sono.

Hakika wewe ni shujaa halisi wa taifa hili, ukiwa Mtanzania wa kwanza kuwa profesional footboler tena ktk level kubwa unapaswa kuenziwa ukiwa hai.
SUNDAY MANARA (WA PILI KULIA) WAKATI AKIKIPIGA ULAYA.

Najua ukitangulia mbele ya haki mengi kukuhusu yatasemwa,hasa historia yako murua ya kandanda lakini mimi mwanao nakuenzi leo na siku zote,naambiwa ww ni best player of all time ktk taifa hili.

Hakika ni kujivunia kunakostahiki kwangu, kitu kikubwa ni kuachia maamuzi yangu ktk mambo makhsuus, kama kuamua kupenda klabu yangu maalum ya Simba SC ilhali wewe ni legend wa Yanga.

Sizisahau zama zile nikilazimisha uninunulie jezi nyekundu na hukusita, naikumbuka pia ile siku niliyotia viatu vyako kwenye pipa la maji,ili tu usichezae ktk game ya Pan African na Simba, but siku zote uliacha mahaba yangu kwa Simba yawe huru. Kila ulichonipa baba nakikumbuka sana,kuanzia shule,madrasa na hata ushauri wako pia....nakupenda mzee wangu na jivunie mimi,
HAPPY BIRTHDAY


Ni mimi mwanao  Haji S.Manara

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV