November 7, 2016



Sasa ni hofu ya kueremka daraja msimu huu tayari imeshaanza kulinyemelea benchi la ufundi la JKT Ruvu kutokana na matokeo mabaya ambayo timu hiyo imekuwa ikiyapata katika mechi zake za Ligi Kuu Bara msimu huu.

JKT Ruvu kabla ya mchezo wake wa jana Jumapili dhidi ya Toto Africans kwenye Uwanja wa Mabatini, ilikuwa imeshinda mechi mbili tu kati ya 14 ilizokuwa imecheza ikiwa imetoka sare sita na kufungwa sita na ilikuwa nafasi ya pili kutoka mkiani.

Mmoja wa viongozi wa benchi la ufundi la JKT Ruvu na ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa timu hiyo, George Minja, ameliambia Championi Jumatatu kuwa, kwa sasa akili zao zimejaa hofu kubwa kama wanaweza kuepukana na balaa la kushuka daraja.

“Mzunguko wa kwanza ndiyo huo unafikia tamati hivi karibuni na nafasi tunayoshika kwenye msimamo ya ligi ni mbaya sana, hakika hali hiyo inatutesa sana, kwani kama tusipokuwa makini tunaweza kushuka daraja.

“Sijui ni nini kilichotukumba kwa sababu hapo mwanzo tulianza vizuri ligi kuu lakini baadaye mambo yamebadilika, hakika inasikitisha sana,” alisema Minja.


JKT tangu ilipopanda daraja, haijawahi kushuka lakini msimu huu hali inaonekana kuwa na hali tete.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic