November 4, 2016Na Mwandishi Wetu, Mbeya
Mabingwa wa soka tanzania Bara, Yanga leo wamefanya mazoezi yao ya mwisho kabla ya kuivaa Prisons kesho.

Mazoezi hayo wamefanya kwenye Uwanja wa Sokoine mjini hapa, tayari kwa mechi hiyo wanayoisubiri kwa hamu baada ya kufanya marekebisho kadhaa kutokana na makosa waliyoyafanya katika mechi iliyopita ambayo walilala kwa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City kwenye uwanja huo.

Hata hivyo, wachezaji wa Yanga ambao walionekana wame relax na wako tayari kwa mechi ya kesho, walifanya mazoezi kwa muda mfupi na baadaye wakanyoosha viungo.

Jana pia ilikuwa hivyo lakini Kocha Hans van der Pluijm akatumia muda mwingi kuzungumza na wachezaji wake.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV