November 4, 2016

MAVUGO

Straika wa Simba, Laudit Mavugo, juzi alishindwa kutumia nafasi kadhaa alizozipata katika mchezo dhidi ya Stand United na kusema kuwa hakuwa na bahati katika mchezo huo.

Mavugo ambaye mpaka sasa ameifungia Simba mabao manne katika Ligi Kuu Bara, alisababisha penalti iliyozaa bao lililoipa ushindi timu yake lakini yeye akashindwa kuonyesha makali yake zaidi ya hapo.

“Mchezo ulikuwa mgumu lakini tunamshukuru Mungu kupata ushindi, nimekosa nafasi kadhaa za kufunga lakini najipanga kwa mechi zijazo na hasa mzunguko wa pili ambao naamini nitarejea katika ubora wangu ili niweze kuisaidia timu yangu kupata matokeo mazuri na kutwaa taji la Ligi Kuu Bara msimu huu,” alisema Mavugo.

Hata hivyo, bado Mavugo ana nafasi ya kufanya vema katika Ligi Kuu Bara kwa kujirekebisha katika mambo kadhaa.

Moja ya jambo analotakiwa kurekebisha ni upotezaji wa nafasi za mabao ambazo amekuwa akipoteza nyingi kutokana na kuwa na papara.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV