November 4, 2016



Huku mkataba wake ukielekea ukingoni, beki kisiki wa Azam FC, Pascal Wawa, raia wa Ivory Coast, ameweka bayana kuwa hana mpango wa kuendelea kuitumikia timu hiyo kufuatia madai ya kukataliwa na kocha mkuu wa timu hiyo, Mhispania, Zeben Hernandez.

Wawa alijiunga na Azam mwaka 2014 kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea El Merreikh ya Sudan kabla ya kuongeza mkataba ambao unamalizika siku chache zijazo huku akiwa hajaichezea Azam mchezo wowote tangu kuanza kwa msimu huu.

Kilichosababisha asicheze mwanzoni mwa msimu huu ni kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya nyama za paja, lakini kwa sasa ameshapona, huku akiachwa jijini Dar kwenye safari ya timu hiyo iliyopo Kanda ya Ziwa.

Taarifa ambazo Championi Ijumaa linazo ni kuwa, beki huyo alipishana kauli na kocha wake huyo katika mazoezi ya timu hiyo na hivyo kuondolewa katika progamu za mazoezi ambapo wakati mwingine kutumika katika sehemu ya kuwabebea maji wachezaji wenzake.

“Wawa ana mpango wa kuondoka kwa sababu hataki kuongeza mkataba kutokana na kutokuwa na maelewano na kocha mkuu, maana kama kupona ameshapona lakini hataki kumtumia,” kilisema chanzo hicho.

Alipotafutwa Wawa alisema: “Sijasafiri na timu, mimi nipo Dar nimepumzika lakini nimeshapona vizuri na sina tatizo lolote ila nadhani tatizo unalifahamu hilo.

“Huyu mwalimu anasema mimi siyo mchezaji mzuri, nasubiri mkataba wangu uishe ili nirudi kwetu nikapumzishe akili kwanza halafu nitajua cha kufanya maana siwezi kuongeza mkataba hapa Azam."

SOURCE: CHAMPIONI 


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic