Baada ya kimya kingi, hatimaye Kocha wa Mbeya City amekata mzizi wa fitina kwa kutoa baraka zote kwa kipa mkongwe, Juma Kaseja kutafuta timu nyingine kwani hatarajii kuwemo kwenye mipango yake ya raundi ya pili.
Phiri amesisitiza kuwa amefikia ‘kunawa’ kwa kipa huyo wa zamani wa Simba na Yanga kutokana na mvutano mkubwa uliopo kati ya kipa huyo na uongozi wa Mbeya City kwa kile kilichotajwa ni ishu ya malipo ya fedha za usajili, mvutano uliosababisha asiwe na msaada wowote mpaka sasa.
Licha ya jina lake kupitishwa kama mchezaji wa Mbeya City msimu huu, Kaseja hakuripoti kikosini tangu kuanza kwa msimu huu Agosti 20, mwaka huu licha ya Phiri kukiri pengo lake kuwepo.
Akizungumza kabla ya kwenda kwao nchini Malawi kwa mapumziko, Phiri hakutaka kupindisha kwa kusema jina la Kaseja halimo kwenye orodha ya wachezaji atakaokuwa nao raundi ya pili huku ripoti yake ikibainisha pia kuhitaji wachezaji saba, akiwemo mbadala wa Kaseja golini.
SOURCE: CHAMPIONI
0 COMMENTS:
Post a Comment