November 7, 2016Mwenyekiti wa Azam FC, Said Mohammed amefariki dunia leo.

Said Mohammed ambaye alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi amefariki dunia baada ya kuugua ghafla na alikimbizwa kwenye hospitali ya Agakhan ambao mauti yalimkuta.


Taarifa kutoka kwa ndugu zake, zimeeleza anatarajia kuzikwa kesho Saa 10 jioni kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

Mwenyezi Mungu amrehemu.

SALEHJEMBE inatoa pole kwa familia ya Mzee Said, Familia ya Azam FC pamoja na wanamichezo hasa wapenda soka wote, sisi sote tu njia moja, hivyo ni vizuri kuweka akiba baada ya duniani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV