November 18, 2016

LWANDAMINA AKIZUNGUMZA NA MWANDISHI WETU, SALEH ALLY

Kiungo na nahodha wa Yanga, Mnyarwanda, Haruna Niyonzima, ametamka kwamba licha ya mabadiliko yaliyofanywa kwenye benchi la ufundi la timu hiyo kwa kumuondoa Mholanzi, Hans van Der Pluijm na kumleta Mzambia, George Lwandamina, kwao hawataathirika kwa jambo lolote na badala yake wataongeza juhudi za kuhakikisha wanachukua ubingwa bila ya kujali watafundishwa na kocha gani.

NIYONZIMA AKIJIFUA

Imeelezwa kuwa Yanga tayari wamemalizana na Lwandamina kwa ajili ya kuchukua mikoba ya Pluijm katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ambapo Mzambia huyo tayari ameshasaini mkataba wa miaka miwili akitokea Zesco ya nchini kwao.

Kiungo huyo aliyewahi kutamba na APR ya Rwanda, amesema kwamba wao hawataangalia ni kocha gani ambaye atawaongoza kwenye mzunguko huo, bali wanachofanya wao ni kutetea taji lao la ubingwa walilotwaa msimu uliopita wakiwa na Pluijm.

“Nadhani tuna nafasi kubwa ya kutetea kombe hilo kwa sababu bado tupo vilevile kama msimu uliopita na hakuna hata mchezaji aliyeondoka na tunajuana kila mtu anavyocheza na tuna morali kubwa ya kutaka kutetea kila kombe letu kwa msimu huu,” alisema Niyonzima.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic