November 20, 2016
Cristiano amefunga mabao matatu, hat trick wakati wa Madrid Derby inayozikutanisha Real Madrid na Atletico Madrid.

Hat trick hiyo ya leo kwa Ronaldo inakuwa ni ya 39 tokea aanze kucheza soka la kulipwa.

Kazi ilikuwa kwenye Uwanja wa Vicente Calderone na Ronaldo akatupia zote tatu Madrid ikiibuka na ushindi wa mabao 3-0 ugenini katika mechi hiyo tamu ya La Liga.

Bao la kwanza alifunga kwa mkwaju wa adhabu, akafunga la pili kwa penalti baada ya kuangushwa na msumari wa mwisho amemalizia pasi safi ya Gareth Bale.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV