November 2, 2016



ALFRED LUCAS MAPUNDA

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limeiambia timu ya Stand United ya mkoani Shinyanga, iache kulalamika hovyo na badala yake icheze soka kwani ndiyo kazi yao pekee.
Kauli ya TFF imekuja baada ya viongozi wa Stand United kulalamika upangaji mbovu wa ratiba ya Ligi Kuu Bara ambapo wanaona inawabana na kuwanyima fursa ya kuonyesha makali yao.

Stand United ambayo Jumapili iliyopita ilicheza dhidi ya Ruvu Shooting na kutoka suluhu kwenye Uwanja wa Mabatini, Pwani, leo Jumatano inatarajiwa kupambana na Simba katika Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

Inacholalamika zaidi timu hiyo ni kwamba, baada ya mchezo wao uliopita, walilazimika kusafiri na kufika Shinyanga siku moja kabla ya mchezo wa leo tofauti na Simba waliokuwa mkoani humo kwa takribani wiki moja.

Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas, amesema : “Unajua ukikaa chini na kusikiliza malalamiko ya kila timu tutajikuta ligi ikimalizika Septemba mwakani na si Mei kama ilivyopangwa, sasa niwaambie tu hao Stand na timu nyingine zenye malalamiko kama hayo ziache kuongea sana, zicheze soka, basi.

“Mbona awali walivyokuwa wakipata matokeo mazuri hawakuwa wakiongea kauli hizo, sasa hivi wanaona wameshaanza kupoteana wanatafuta visingizio, ratiba imepangwa na kila mmoja aliiona kabla, sasa iweje malalamiko yaje sasa hivi?”


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic