November 2, 2016



Hii si taarifa nzuri kwa kuwa, beki wa Yanga, Juma Abdul anaweza asionekane kwenye michezo ya Ligi Kuu Bara mpaka Januari, mwakani kutokana na majeraha ya nyonga yanayomsumbua kwa sasa.

Beki huyo ambaye alipata majeraha hayo Oktoba 16, mwaka huu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam, bado anaendelea na matibabu huku Yanga ikibakiwa na mechi tatu kabla ya mzunguko wa kwanza kumalizika na mzunguko wa pili ukitarajiwa kuanza Januari, mwakani.

Daktari wa Yanga, Edward Bavu, amesema: “Juma yupo katika uangalizi maalum kuhakikisha anakuwa fiti ndiyo aanze mazoezi, tangu alipoumia hakuwa akifanya mazoezi.
“Kwa sasa tunaangalia maendeleo yake kabla ya kurudi uwanjani rasmi, kama akionekana bado ataendelea kukaa nje mpaka pale tutakaporidhika juu ya afya yake,” alisema Bavu.

Hata hivyo pamoja na daktari huyo kusema hivyo kumekuwa na hofu kubwa kuwa beki huyo hataweza kurudi uwanjani hadi Januari mwakani, kutokana na mechi tatu zilizobaki za mzunguko wa kwanza kuwa karibukaribu.

Yanga wanacheza na Mbeya City, halafu watavaana na Mbeya City wikiendi ijayo na mwisho watamaliza na Ruvu Shooting.

Mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara unatarajiwa kumalizika Jumapili ijayo lakini viporo vitaenda hadi Novemba 13.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic