November 16, 2016Kampuni ya StarTimes imezidi kupaa kiteknolojia baada ya kuzindua runinga mpya ambazo hazihitaji king'amuzi.

Runinga hizo zenye ukubwa wa Inchi 40, 32 na 24 zina king'amuzi ambacho kinakuwa ndani yake.


Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo unaofanyika jijini leo usiku, Mkurugenzi Mtendaji wa Star Media Limited, Star Media Tanzania Limited, Lanfang Liao alisema kuwa lengo la kampuni yake kuleta runinga ya aina hiyo ni kukidhi mahitaji ya Watanzania hasa wenye kipato cha kawaida na chini.

"Lengo letu ni kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuleta maendeleo kwa wananchi. Luninga hii itasaidia watazamaji kukidhi mahitaji yao kwa chaneliza ndani na zile za kimataifa," alisema Liao.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano Teknolojia na Uchukuzi, Marian Sasabo ambaye pia aliwapongeza StarTimes kwa uzinduzi wa runinga hizo za kisasa ambazo zina warrant ya mwaka mzima.


1 COMMENTS:

  1. Runinga hizo zenye ukubwa wa Inchi 40, 32 na 24 zina king'amuzi ambacho kinakuwa ndani yake.
    SAWA KING'AMUZI KIPO NDANI YAKE SITANUNUA JE VIPI ANTENA AU DISH LA STAR TIMES SITAKIWI KUNUNUA ?

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV