Mshambuliaji hatari wa Athletic Bilbao, Aritz Aduriz ameonyesha umri si jambo baya katika soka na una faida baada ya kufunga mabao yote matano wakati timu yake ilipoimaliza KRC Genk ya Ubelgiji kwa mabao 5-3.
Ilikuwa ni mechi ya Kombe la Europa na Mtanzania Mbwana Samatta alikuwa uwanjani hadi Aduriz alipofunga bao lake la 4 katika dakika ya 74 na akatika katika dakika ya 83.
Mechi ilikuwa ngumu kwa kila upande Aduriz mwenye umri wa miaka 35 alipotupia bao katika dakika ya 8 na kuongeza tena katika dakika ya 24 lakini Genk wakajibu kwa kupata bao kupitia Leon Balley raia wa Jamaica.
Wakati ikionekana kuwa mapumziko itakuwa 2-1, Aduriz alipachika tena bao katika dakika ya 44 na kufanya hadi mapumziko iwe wenyeji wako mbele kwa mabao 3-1.
Kipindi cha pili, Genk walionekana wamepania baada ya kupata bao kupitia kiungo wake Onyinye Ndidi na Aduriz akaongeza bao la nne katika dakika ya 74 na kuwavunja nguvu Genk.
Samatta akitoka katika dakika ya 83 na kumuachia Nikos Karelis kumalizia dakika saba zilizobaki lakini Aduriz akashindilia msumari wa mwisho katika dakika ya 90.
0 COMMENTS:
Post a Comment