November 16, 2016


Straika wa Yanga, Amissi Tambwe mwenye mabao saba, ameibuka na kusema kuwa, alikuwa na presha kuona wapinzani wao Simba wamewazidi pointi nyingi, lakini sasa presha yake imeshuka.

Awali, Simba ilikuwa juu ya Yanga kwa pointi nane, lakini mzunguko wa kwanza umemalizika wakiwa kwa tofauti ya pointi mbili.

Tambwe alisema mzunguko wa kwanza ulikuwa mgumu kiasi cha kuwachanganya zaidi kufuatia kupishana pointi nyingi na wapinzani wao, lakini wamepata faraja kufuatia wapinzani wao hao kupoteza michezo miwili mwishoni.

“Mzunguko wa kwanza ulikuwa na ushindani wa hali ya juu na ulikuwa mgumu sana kutokana na wapinzani wetu kutupita pointi nyingi zilizotufanya tupigane kufa na kupona hadi hapo tulipofikia.

“Lakini tunashukuru Mungu kuona tumewasogelea na kubakiza pointi mbili tu ila sasa hivi afadhali naweza kutembea kwa furaha,” alisema Tambwe.


2 COMMENTS:

  1. Yani wachezaji wa yanga kutwa kuizungumzia simba sc mbn wachezaj wa simba sc cjawackia wakiropoka ropoka hvyo kwny vyombo vya have kuhusu yanga.... Km huyu tambwe, niyo, msuva, bossou, mocha wao wao ni simba sc tu kila wakiongeo kwny vyombo vya hbr

    ReplyDelete
  2. tuwekee kwenye youtube maneno yao kwamba yanga wanawazungumzia zaidi simba. mbona simba kila mliposhinda mechi zenu ilikuwa kila siku maneno hayaishi, mara "huu msimu wetu yanga msisumbuke" huku "yanga mlizoea kubebwa sasa tumekuja wazee wa kazi" leo mnaanza kusema wachezaji wa yanga wanawasema, kijana acha uongo, kama huyo tambwe, bossou ndo huwa hawana muda wa kubwata, pia laumu waandishi wanaoenda kutafuta habari kwake kwa kuwahoji juu ya watani wao.
    ni mawazo tu kijana

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV