November 13, 2016


Baada ya Simba kupoteza mechi mbili mfululizo za Ligi Kuu Bara, wadau mbalimbali wa timu hiyo wameushauri uongozi wa benchi la ufundi la Simba kumpa nafasi kipa Peter Manyika.

Wadau wamedai Manyika amekuwa akiozea benchi wakati kipa mkongwe, Vicent Angban akiendelea kudaka.

Kupitia wadau hao waliotuma ujumbe kupitia email ya salehkubwa@gmail.com, wamelalama kwamba Angban anaweza kuwa amechoka kutokana na kudaka mfululizo.

Wengi wametaka kuwe na utoaji nafasi angalau kipa huyo mkongwe kudaka mechi tatu na Manyika akadaka moja ili kuepuka kuua kipaji chake.

Hata hivyo, inaonyesha wengi wao walikerwa na kipa huyo kufungwa mabao mawili  dhidi ya Prisons ambayo wao waliyaita ‘rahisi’


Hadi inafikisha mechi 13, Simba ilikuwa inaongoza kwa tofauti ya pointi nane, lakini baada ya kufikisha mechi 15, Simba imebaki inaongoza pointi mbili. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV