November 12, 2016


Kocha Jose Mourinho amekubali kumwaga kitita cha euro milioni 15 ili kwa kiungo Mesut Ozil (28) ili atue Old Trafford na kujiunga na Man United.

Mourinho ambaye aliwahi kufanya kazi na Ozil wakiwa Real Madrid, yuko tayari kumwaga kitita hicho ili kumnasa Ozil raia wa Ujerumani mwenye asili ya Uturuki ambaye ni tegemeo kubwa katika kikosi cha Arsenal ya mzee Arsene Wenger.

Taarifa za ndani kutoka Manchester United, zimeeleza, Mourinho anaamini hiyo ni ofa bora kumpa Ozil na kila kitu kitakwenda vizuri kama Mjerumani huyo, hataingia mkataba mpya na Arsenal.

Kuhusiana na mshahara imeelezwa itakuwa ni euro 290,000 euro kwa wiki kwa kuwa sasa ndiye mchezaji anayelipwa zaidi Arsenal.


Taarifa za awali zimeeleza kwamba Arsenal kama wataongeza naye mkataba walikuwa tayari kumlipa euro 185 kwa wiki, ikiwa wameongeza euro 20,000 kwa kila wiki, yaani euro 80,000 kwa mwezi zikiwa ni sehemu hiyo ya nyongeza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV