November 10, 2016


FULL TIME
 
Mwamuzi anamaliza mchezo Yanga inapata ushindi wa mabao 2-1.
 
Dakika ya 90 + 4: Muda wowote mchezo unaweza kumalizika.
 
Dakika ya 90: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 2 za nyongeza.

Dakika ya 89: Yanga wanamiliki mpira muda mwingi.

Dakika ya 88: Yanga wanafanya mabadiliko, anatoka Ngoma anaingoa Matheo. 

Dakika ya 87: Said Dilunga anapewa kadi ya njano kwa kucheza faulo. 

Dakika ya 75: Yondani anazungumza na refa akilalamika kilichotokea kuwa Dante alifanyiwa faulo.
 
Dakika ya 74: Ruvu wanafanya shambulizi lakini kipa wa Yanga, Kakolanya anaudaka. Wakati huo Dante yupo chini akipatiwa matibabu baada ya kuumia wakati akiwania mpira.

Dakika ya 68: Tambwe anatupia mpira wavuni lakini mwamuzi anapuliza kipenga kuwa ameotea.
 
Dakika ya 58: Yanga wanaongoza ambao 2-1.
 
Dakika ya 52: Yanga wanapata bao la pili mfungaji akiwa ni Niyonzima. Kazi nzuri iliyofanya na Ngoma ambaye aliubabatiza mpira kisha akampa pasi Niyonzima akapiga shuti na kujaa wavuni.
 
GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!!

Dakika ya 50: Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi amesimama anatoa maelekezo baada ya bosi wake Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Pluijm kupelekwa kwenye benchi na mwamuzi kutokana na kupishana kauli.
 
Dakika ya 48: Chirwa anapata nafasi, anapiga shuti lakini linapaa juu ya lango la Ruvu.

Dakika ya 46: Kipindi cha pili kimeanza.

HALF TIME
Kipindi cha kwanza kimekamilika. Mwamuzi amepuliza kipenga timu zote zimeenda kupumzika.

Dakika ya 45: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika mbili za nyongeza.

Dakika ya 44: Yanga wanatoa, Ruvu wanarusha lakini Msuva anaunasa na kuelekea kwa wapinzani.
 
Dakika ya 40: Timu zote zinashambuliana kwa zamu. 

Dakika ya 34: Yanga 1, Ruvu 1
 
Dakika ya 32: Simon Msuva anaipatia Yanga bao la kusawazisha, kazi nzuri iliyofanywa na Niyonzima kisha akatoa pasi kwa Msuva ambaye aliumalizia mpira wavuni baada ya mabeki wa Ruvu kujichanganya.
 
GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO!

Dakika ya 28: Msuva anaingia na mpira lakini Ruvu wanaokoa na inakuwa kona.

Dakika 25: Yondani anapanda na mpira lakini anazuiwa na mabeki wa Ruvu na mpira unatoka nje, unakuwa wa kurushwa.

Dakika ya 20: Yanga wanafanya shambulizi kali, Chirwa anapata nafasi lakini anashindwa kufunga, inakuwa kona.
 
Dakika ya 15: Yanga wanacheza kwa kasi na kuonekana kutafuta bao lakini wapinzani wao wanawapa wakati mgumu.
 
Dakika ya 12: Ngoma anapata nafasi langoni kwa Ruvu lakini anashinwa kutumia.

Dakika ya 9: Ruvu wanaongoza bao 1-0. Yanga wanaonekana kuchangamka.

Dakika ya 8: Ruvu wanaparta bao la kwanza kupitia kwa Mussa, alipata mpira kutoka upande wa kushoto kwa Yanga na kupiga shuti kali ambali lilimshinda kipa wa Yanga.
 
GOOOOOOOOOOOOOOOO!!!
 
Dakika ya 5: Timu bado zinasomana, Yanga wamepata kona wameshindwa kuitumia vizuri, Ruvu nao wamefika langoni kwa Yanga lakini hawakuwa na madhara.
 
Dakika ya 1: Mchezo umeanza.

Timu ndiyo zinaingia uwanjani muda huu.

Tayari timu zimeshapasha misulu moto na wachezaji wameingia vyumbani kwa ajili ya kurejea kuja kuanza mchezo huu wa Ligi Kuu Bara kati ya Yanga dhidi ya Rucu Shooting.

Kikosi kamili cha Yanga ambacho kinatarajiwa kuanza kwenye mchezo wa leo hiki hapa:
1. Beno Kakolanya
2. Hassani Kessy
3. Mwinyi Haji
4. Kelvin Yondani
5. Andrew Vicent
6. Thabani Kamusoko
7. Saimoni Msuva
8. Haruna Niyonzima
9. Donald Ngoma
10. Amisi Tambwe
11. Obrey Chirwa

Akiba
- Deogratius Munishi
- Pato Ngonyani
- Oscar Joshua
- Deusi Kaseke
- Juma Mahadhi
- Saidi Juma
- Anthony Mateo

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV