November 13, 2016


Dakika ya 90 + 4: Mwamuzi anamaliza mchezo, Zimbabwe 3, Tanzania 0. Ulikuwa mchezo wa kirafiki wa kimataifa.
 
Dakika ya 90 + 3: Mvua inaendelea kunyesha uwanjani hapa.
 
Dakika ya 90 + 1: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika nne za nyongeza.
 
Dakika ya 90: Zimbabwe wanatupia mpira wavuni lakini mwamuzi anakataa kwa kuwa mfungaji alifanya faulo kabla ya kufunga.
 
Dakika ya 88: Stars wanafanya shambulizi kali, Dante anapiga kichwa, beki wa Zimbabwe anaokoa mpira kwenye mstari.
 
Dakika ya 87: Zimbabwe wanafanya shambulizi lakini washambuliaji wao wanakosa umakini na kushindwa kufunga.
 
Dakika ya 85: Bado hali si shwari kwa Taifa Stars, Zimbabwe wamemiliki mpira muda mwingi.
 
Kumbukumbu ya kikosi cha TAIFA STARS kilichoanza katika mchezo huu:
1. Aishi Manula
2. Michael Aidan
3. Mohamed Hussein
5. Erasto Nyoni
4. Andrew Vicent
6. Himid Mao
7. Msuva
8. Mzamiru Yassin
9. Mbwana Samatta
10. Maguri
11. Kichuya


Dakika 80: Zimbabwe bado hawatoki langoni mwa Taifa Stars, mabadiliko yaliyofanyika hayajawa na faida kubwa.
 
Dakika ya 78: Mchezo bado unaendelea kwa kasi.
 
Dakika ya 72: AnatokaElius Maguri anaingia John Bocco.

Dakika ya 69: Taifa Stars inafanya mabadiliko, anatoka Simon Msuva anaingia  Thomas Ulimwengu. Anatoka Yassin Mzamiru anaingia Mohamed Ibrahim.
 
Dakika ya 68: Mchezo unaendelea kwa kasi.

Dakika ya 65: Matokeo bado ni 3-0, Taifa Stars bado wamezidiwa, Zimbabwe wanamiliki mpira muda mwingi.
 
Dakika ya 56: Zimbabwe wanapata bao la tatu mfungaji ni
Mushekwi baada ya mpira wa faulo uliopigwa kutoka upande wa kulia kupita moja kwa moja mpaka wavuni.


GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!!

Dakika ya 54: Tanzania bado wanaonekana hawajakaa sawa na pasi zao hazijaeleweka.
 
Dakika ya 53: Zimbabwe wanapata bao la pili kupitia kwa
Rusike Mathew baada ya kucheza pasi kadhaa kuanzia pembeni ya uwanja hadi katikati kisha kupiga shuti kali linalojaa wavuni.

 
GOOOOOOOOOOOOOOO!!

Dakika ya 52: Zimbabwe wanacheza vizuri kwa kugongeana, wanafanya shambulizi lakini Manula anauwahi mpira na kuudaka.


Dakika ya 47: Zimbabwe wanafanya shambulizi kali, linapigwa shuti kali kutoka nje ya 18, kipa wa Stars, Aishi Manula anafanya kazi nzuri ya kulipangua shuti, inakuwa kona ambayo haizai matunda.
 
Dakika ya 46: Kipindi cha pili kimeanza.
 
HALF TIME
 
 
Dakika ya 45 + 2: Mwamuzi anapuliza kipenga kumaliza kipindi cha kwanza. Wenyezi Zimbabwe wanaongoza bao 1-0.
  
Dakika ya 45: Mwamuzi wa pembeni anaonyesha dakika mbili za nyongeza.
 
Dakika ya 44: Dante wa Stars anafanya kazi nzuri kwa kublock mpira wa krosi ulipigwa kuelekea langoni mwa Stars.

Dakika ya 42: Uwanja ulilowa maji na ulionekana ukiwapa wakati mgumu wachezaji wa Stars dakika za mwanzoni, lakini sasa wameuzoea na wanacheza kwa kuelewana.
 
Dakika ya 40: Mashambulizi bado ni ya kupokezana, Mbwana Samatta wa Stars anarudi mpaka kwenye kiungo kusaidiz kuchukua mipira.
 
Dakika ya 30: Bado mchezo ni mkali, timu zote zinashambuliana kwa zamu.

Dakika ya 22: Matokeo bado Zimbabwe inaongoza bao 1-0 dhidi ya Taifa Stars.

Dakika ya 10: Stars wanaonekana kutulia na kuanza kujipanga, wanafanya shambulizi kali kwa krosi kutoka kulia kutua kichwani kwa Eliasi Maguri ambaye anapiga kichwa kikali kinatoka nje ya lango la Zimbabwe.

Dakika ya 9: Knowledge Musona anaipatia Zimbabwe bao baada ya mpira wa krosi kupigwa kutoka kulia mwa uwanja kisha kugongwa kichwa na mwenzake, wakati huo beki wa kati wa Stars, Erasto Nyoni aliruka juu lakini akashindwa kuuzuia mpira, hivyo, Musona akamalizia kazi kiulaini.

Dakika ya 7: Zimbabwe wanaendeleza mashambuliz makali langoni mwa Stars na kuwapa wakati mgumu mabeki wa Stars kuokoa.

Dakika ya 1: Mchezo umeanza kwa kasi, Zimbabwe wanafanya mashambulizi mengi langoni mwa Taifa Stars.

Mchezo huu wa kirafiki unachezwa nchini Zimbabwe.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV