November 13, 2016Na Mwandishi Wetu, Mwanza
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye amesema Uwanja wa Nyamagana ambao umewekewa nyasi bandia ni juhudi za watu kadhaa, lakini kodi ya wananchi wa mkoa wa Mwanza ndiyo iliyotoa mchango mkubwa kufikia ulipo sasa.

Nape ameyasema hayo leo wakati wa ziara yake ya kuutembelea uwanja huo iliyofanyika leo jijini hapa baada ya serikali ya awamu ya tano kuonyesha juhudi za makusudi kuhakikisha suala la upatikanaji wa nyasi bandia, zinatolewa bandarini na kuwekwa kwenye uwanja huo linafanikiwa kwa wakati mwafaka ili Mwanza na mikoa ya jirani ijiendeleze kimichezo na hasa soka.


Akizungumza na SALEHJEMBE wakati wa mkutano huo wa waandishi wa habari, Nape ambaye ameonyesha kufuatilia mambo mengi ya michezo kwa ukaribu, amesema wanaoutumia uwanja huo kama kampeni za kuwania uongozi hawako sawa kwa kuwa si uwanja wa mtu, badala yake ni uwanja wa Wanamwanza.

“Huu ni uwanja wa Wanamwanza wote, mama mtilie, wachuuzaji wa vitu barabarani na wengine wamelipa kodi yao na serikali imeitumia katika ununuzi wa nyasi bandia.

“Nyasi hizo zilikwamba bandarini kutokana na suala la kodi. Lakini mwisho, serikali ikashirikiana na TFF na kuzitoa na kazi ya uwekaji nyasi hizo hii inakwenda ukingoni,” alismea.


Hivi karibuni, kumekuwa na baadhi ya viongozi wa TFF na wale wa vyama vya soka katika mikoa, wakiutumia kama sehemu ya kampeni zao za kuwania kupata uongozi.

Pamoja na kutembelea uwanja huo, Nape aliwataka Wanamwanza kuutunza na kuudhamini kama sehemu ya moja ya maendeleo.

Aidha, alisisitiza Serikali itaendelea kuwekeza kwa kufanya ukarabati kwenye viwanja mbalimbali nchini ili kuviboresha na kusaidia kusukuma maendeleo ya michezo kwa haraka zaidi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV