Mshambuliaji nyota wa zamani wa Inter Milan, Adriano alirejea tena San Siro usiku wa kuamkia leo na kupewa heshima ya kuwaaga mashabiki wa klabu hiyo.
Mashabiki walikuwa kibao wakati Inter Milan ikiivaa Lazio na kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 na walimshangilia kwa nguvu naye akionekana akiwa na furaha sana.
Adriano raia wa Brazil, alikuwa tegemeo wa Inter Milan 2001 hadi 2002 halafu akarejea tena na kuitumikia kuanzia 2004 hadi 2009 alipoondoka na kujiunga Sao Paolo kwa mkopo.









0 COMMENTS:
Post a Comment