December 22, 2016



Mabingwa wa Soka Tanzania Bara, Yanga leo wataendelea na mazoezi kwa mara ya pili ikiwa ni baada ya kugoma siku mbili.

Wachezaji wa Yanga waligoma kufanya mazoezi kwa madai kuwa hawajalipwa mshahara wao wa mwezi uliopita.

Lakini, jana jioni walirejea mazoezini baada ya kuwa wamezungumza na uongozi na kukubaliana kuwa watamalizana.


Leo wanaendelea na mazoezi kwa mara ya pili ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi yao dhidi African Lyon ambayo itapigwa kesho Ijumaa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic