December 30, 2016



Mshambuliaji ya Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe, amesema kuwa hivi sasa hataki mchezo anapokuwa uwanjani akiitumikia timu yake, hivyo wapinzani wao katika Ligi Kuu Bara msimu huu wakae tayari kuwapisha katika nafasi yao ya kwanza.

Yanga kwa sasa ipo nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu ikiwa na pointi 40, nyuma ya Simba ambayo ina pointi 41 kabla ya mchezo wa jana dhidi ya Ruvu Shooting.

Tambwe ambaye juzi Jumatano alifanikiwa kufikisha mabao tisa katika ligi ya msimu huu, alisema kuwa kasi kubwa ambayo walionyesha katika mchezo dhidi ya Ndanda FC anaamini ilikuwa ni ya kawaida sana kuliko ile watakayokuja nayo kwenye mechi zao zinazokuja pia na yeye hivi sasa anakuja kivingine.

“Wapinzani wetu wajiandae kwelikweli kutuzuia katika mechi zetu zijazo kwani kasi tutakayorudi nayo itakuwa ni moto wa kuotea mbali zaidi ya ile tuliyoionyesha dhidi ya Ndanda FC ambapo tulishinda mabao 4-0.

“Nasema hivyo kwa sababu sioni sababu ambayo itatufanya tushindwe kufanya hivyo na ukizingatia tuna kikosi kizuri, hivyo wapinzani wetu wajiandae na wakae tayari kutupisha katika nafasi yetu hiyo.


“Baada ya mapumziko ya nusu msimu, kwa sasa nimekuja kivingine, nikishindwa kufunga basi ni lazima nitengeneze nafasi ya bao, hiyo ni kuhakikisha tunarudi katika nafasi yetu ya kwanza ambayo tumewaachia Simba kwa muda mrefu,” alisema Tambwe.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic