December 30, 2016


Wakati Simba ikiwa katika mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Bara, upande wa pili, Mkurugenzi wa Ufundi wa Yanga, Hans van Der Pluijm, amekiri kuwa anazifuatilia timu za ligi kuu ikiwemo Simba ili kujua mbinu zao na kuiwezesha Yanga ifanye kweli pindi itakapokutana nazo. 

Chanzo cha swali kwa bosi huyo ni kutokana na uwepo wake uwanjani wakati Simba ilipoifunga JKT Ruvu bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Jumamosi iliyopita, ambapo Pluijm alikuwa bize akiandika mambo kadha awakati mchezo ukiendelea akiambatana na Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh.

Akizungumzia uwepo wake uwanjani hapo wakati wapinzani wao wakicheza, alisema: “Moja ya majukumu yangu kwa sasa ni kuhakikisha nafuatilia timu nyingine.

“Ninatakiwa kuangalia mechi nyingi kadiri iwezekanavyo na nitaendelea kufanya hivyo kwa kuangalia viwango vya wachezaji kwa mmojammoja, sifanyi hivi kwa timu moja, ni kwa timu zote. Wachezaji wengi wamekuwa wakishindwa kudumu kwenye viwango vyao na jinsi wanavyocheza.” 

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic