December 22, 2016


Mario Balotelli haishi vituko, maana jana kalambwa kadi nyingine nyekundu nchini Ufaransa.

Sare ya bila mabao dhidi ya Bordeaux imeifanya Nice kupanda kileleni mea Ligi Kuu Ufaransa. Lakini dakika za majeruhi, Balotelli akalambwa kadi nyekundu.

Awali alianza vituko dhidi ya wachezaji wa Bordeaux, lakini baadaye akanaswa baada ya kumkwatua mshambuliaji wa timu hiyo kwa makusudi.

Wakati mwamuzi akimsogelea, Balotelli alionyesha ishara ambayo ilimkera mwamuzi na baadaye kuna mane no kama walizozana na akalambwa kadi nyekundu moja kwa moja.


Balotelli ndiyo alikuwa amerejea uwanjani mechi kadhaa baada ya kuwa nje muda kadhaa baada ya kulambwa tena kadi nyekundu.








0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic