Bao lililofungwa na Mzamiru Yassin katika mchezo dhidi ya JKT Ruvu, limeifanya Simba kuwa na uhakika wa kumaliza mwaka 2016 ikiwa kileleni kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.
Simba ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya timu hiyo lakini bao hilo lililalamikiwa kinoma. Bao hilo limezua utata huku mijadala ikiendelea kutawala vijiweni na kwenye mitandao ya kijamii kutokana na mazingira yake, lakini mwamuzi mkongwe nchini, Osman Kazi, ameamua kufunga mjadala.
Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Simba ilichomoza na ushindi huo kwa bao pekee la Mzamiru Yassin aliyeunganisha kwa kichwa mpira wa mbali uliopigwa na straika mpya, Pastry Athanas huku lango likiwa tupu kwani kipa wa JKT, Hamisi Seif alikuwa akigaragara chini kwa kile kilichohisiwa kuugulia maumivu lakini mwamuzi akapeta na Simba kutumia mwanya huo kujipatia bao.
JKT Ruvu wakiongozwa na kocha wao, Bakari Shime, walikuwa wa kwanza kulalamikia uhalali wa bao hilo na kwamba mwamuzi Hans Mabena kutoka Tanga alitakiwa kutoa maamuzi ya kiungwana ‘fair play’ kwani kipa huyo aliguswa na Shiza Kichuya akiwa ndani ya eneo la hatari kabla ya kufungwa kwa bao, kabla minong’ono haijahamia kwenye mitandao ya kijamii.
Aidha, mwamuzi wa zamani, Osman Kazi, amelitolea ufafanua kwa kusema: “Ndani ya 18 (eneo la penalti) kuna boksi linaitwa eneo la goli, sisi tunaliita sita, sawa, hapo kwenye sita mara nyingi kipa anapewa kipaumbele zaidi kuliko akiwa nje ya sita.
“Hapo lazima uangalie Kichuya alikuwa kwenye nafasi ipi wakati kipa anaruka kuupiga mpira, pili, pia uangalie kabla ya tukio hilo kipa alilala mara mbili bila kuguswa na mtu yeyote. Hii inaeleza nini kuhusu fitness (utimamu) wa huyo kipa kwenye mchezo wa leo (juzi)? Vitu hivi huwa tunavizingatia katika kutoa maamuzi yoyote yale,” alinukuriwa Kazi.
Kipa huyo mara kadhaa alilalamikiwa na mashabiki wa Simba kwa kupoteza muda kwani alikuwa akianguka bila kusugwa na kulazimika jopo la tiba la klabu hiyo kuingia kumtibu.
Ushindi huo uliifanya Simba kuongoza ligi kwa tofauti ya pointi nne dhidi ya Yanga yenye pointi 39 baada ya mechi 17 kila moja.








Point 39 wamezitoa wapi yanga..afu utasemaje refa kapeta..kazi yako ni kulipoti kilichojiri sio kutafsiri, hauna taaluma ya kukulinda
ReplyDelete