December 26, 2016



Baada ya kuwepo kwa pengo la pointi nne kati ya kikosi cha Simba na Yanga, Kocha Msaidizi wa Simba, Mganda, Jackson Mayanja, amepeleka dongo kwa wapinzani wao Yanga kwa kuwaambia sasa wafute ndoto zao za kutetea ubingwa kwani kikosi hicho hakitaweza kudondosha hata pointi kwenye mechi zake zilizobakia.

Simba inayofundishwa na Mcameroon, Joseph Omog, inaziburuza timu zote 15 ikiwa kileleni na piointi zake 41, nne mbele ya Yanga ambao wana pointi 37 wakiwa kwenye nafasi ya pili.

Mayanja amesema kuwa awali walikuwa na presha kutokana na idadi ya pointi mbili iliyokuwa baina yao lakini sasa wana uhakika wa kufanya vizuri katika mechi zao kutokana na kucheza bila ya kuwaza wapinzani wao kwenda kileleni baada ya mechi moja tu.

“Ni jambo zuri kuona tumeendeleza idadi ya pointi baina yetu na wanaotufuatia Yanga ambapo sasa tuna tofauti ya pointi nne ambazo zinatupa nafasi ya kucheza mechi zetu na kupata ushindi bila ya kuwa na presha kama ilivyokuwa kwenye mechi zetu zilizopita.


“Niwaambie Yanga kwamba kwa jinsi ilivyo wafute ndoto za kutetea ubingwa wao kwani lengo letu ni kuona tunaendeleza wimbi la ushindi katika kila mchezo wetu unaokuja na sisi tupate kutwaa ubingwa baada ya kukaa misimu kadhaa sasa bila ya kuchukua taji hilo,” alisema Mayanja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic