Kampuni ya StarTimes Tanzania, inaendesha Kipindi cha Chemsha Bongo ambapo wateja wake watatakiwa kupiga simu na kujibu maswali mbalimbali kuhusu huduma na bidhaa zao na atakayejibu kwa ufasaha atajishindia runinga mpya ya kisasa kutoka StarTimes.
Chemsha Bongo hiyo itachezeshwa kila Jumatano saa 2:30 hadi saa 2:45 usiku kupitia runinga ya TV1 na kurudiwa siku ya Alhamisi Channel Ten saa 4:00 usiku ambapo wateja wataweza kujinyakulia runinga ya kisasa msimu huu wa Krismasi.
Kampuni hiyo itatoa runinga tano za inchi 24 na 32 kila wiki kwa wiki nne ili wateja wengi zaidi waweze kujishindia na kupata nafasi ya kujionea ubora wa bidhaa zao, hasa runinga za kisasa zenye kinga’muzi ndani yake na zenye kutumia umeme mdogo ili kumpunguzia gharama mteja.
Mteja atatakiwa kujibu maswali na akipatia, basi atajipatia zawadi yake ndani ya wiki mbili. StarTimes imewataka wateja wake kufuatilia kipindi hicho kwani wataweza kufahamu ni maswali gani yanayoulizwa na kuweza kujiandaa kwa kipindi kinachofuata.
Kupitia runinga hizo watakazojishindia pia watapata fursa ya kuona vipindi mbalimbali kama tamthilia za Duty, Diary of Superstar na muziki ambazo hupatikana kwenye Star Swahili.
Pia wataona mpira live kupitia Wold Football Channel ambazo huonesha Bundersliga, Ligue 1, Serie A na European Qualify, vilevile vipindi vya watoto kwenye chaneli ya Nickelodeon, Jim jam na Baby TV.








Kiwanda kimejengwa 2013 A
ReplyDeleteKiwanda kilijengwa 2013 A
ReplyDelete