Unaweza kusema kweli Simba imepania kweli kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara na kurejesha heshima yake.
Kwani pamoja na kuleta wachezaji wawili kutoka Ghana, Kocha wa Makipa, Iddi Salim kutoka Kenya ametua nchini leo.
Salim ambaye ni kocha mwenye cheti cha kazi hiyo kinachotambulika na Shirikisho la Soka Ulaya (Eufa), ametua nchini leo tayari kumalizana na Simba.
Awali, Blog hii ilikuandikia kuhusiana na ujio wa Idd ambaye aliwahi kuinoa Simba wakati Kocha Mkuu akiwa na Dylan Kerr.
Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Iddi alipokelewa na mmoja wa maofisa wa Simba na kutoweka uwanjani hapo.
Salim amewahi kufanya kazi na Gor Mahia ya Kenya kwa mafanikio makubwa, baadaye akafanya kazi na Harambee Stars kabla ya kujiunga na Simba halafu akaenda barani Ulaya kuendelea na kazi pamoja na kujiendeleza kitaaluma.
0 COMMENTS:
Post a Comment